Description
Mhandisi Maselu ni mfano bora wa mwanataaluma ambaye amefanikiwa kujinyanyua kiuchumi kwa kuegemea maadili na
mwenendo wa uwazi na uwajibikaji kazini na katika familia yake. Mwanawe Tony anamhusudu babake na kufanya juu chini kufuata nyayo zake. Lakini tajiriba anazokumbana nazo maishani zinamfunza kwamba dunia rangi rangile. Maisha hayatabiriki, na kamwe, binadamu hana uwezo wa kuyadhibiti na kuyaelekeza apendavyo. Tunaelezwa hadithini:
?Yote aliyotumai kufanikisha yalimponyoka kama tufe lililopakwa mafuta na kutoweza kushikika mikononi. Kupata ajira likawa jambo lenye utelezi ambao kamwe hakuutarajia?.
Nini hatima ya Tony Maselu katika hali hii? Isome riwaya hii ya kusisimua upate jawabu la swali hili.
Reviews
There are no reviews yet.