Description
Kamusi rasmi ya picha imeandikwa kwa upekee usiodhihirika katika kamusi nyingine. Kamusi hii ina sifa zifuatazo:
?
Imeepuka mpangilio wa kialfabeti uliotumiwa na kamusi nyingine. Msamiati umepangwa kwa makundi badala ya kialfabeti kwa sababu wanafunzi katika kiwango hiki bado hawawezi kusaka msamiati kialfabeti (kiabjadi).
?
Mkusanyiko wa msamiati unaambatana na ule ulio katika silabasi ya Kiswahili iliyoidhinishwa na taasisi ya elimu nchini (awali Kenya Institute of Education, sasa Kenya Institute of Curriculum Development).
?
Kamusi hii ina picha maridadi zinazomvutia mwanafunzi na kumrahisishia kazi.
?
Picha zote zimeambatanishwa na maelezo kabambe na kwa lugha nyepesi inayomfaa si mwanafunzi pekee bali mtu yeyote akipendaye Kiswahili.
?
Msamiati uliotumika utamwezesha mwanafunzi kujua mengi kwenye mazingira yake.
Reviews
There are no reviews yet.