Description
Gonzale na kayamba ni vijana barobaro wanaoishi Mombasa katika nyumba ya baba yao aliyestaafu na kuguri shamba. Baba yao amejitoa mhanga kuhakikisha kwamba vijana hawa wanapata masomo ili wabadili mustakabali wa maisha yao na ya familia yao. Asichokijua ni kwamba kuishi kwa vijana mombasa ni ngoma! kuna vishawishi vya kila nui.
Raha inamnogea Gonzale. anaingia katika mapenzi na msichana mrembo wa kitajiri, Brenda. Brenda anapopata ujauzito, kitumbua chake kinaingia mchanga. Kwa Kuwa Gonzale hawezi kumkabili baba yake Brenda, anachana mbuga. Mambo yanapochacha, Brenda anatorokea Nairobi anakomsingizia mwanaume mwingine mimba yake. Je, mwanaume huyu ataikubali mimba hii? Je, Gonzale atanusurika adhabu ya babake Brenda? Lakini makosa ni ya nani? Ni ya mwenye kupenda au mwenye kupendwa?
Reviews
There are no reviews yet.