Description
Kizazi cha leo kimejaa unafiki. Wengi wanapoajiriwa wanajidai ni wafanyakazi waadilifu na wenye bidii kwelikweli. Kumbe wao ni
vinyonga wanaogeuza rangi ili wawasaliti marafiki na kuwaibia waajiri wao! Hawana uaminifu wala huruma wanapotekeleza vitendo vya kifisadi. Uadilifu, wema na utu ni misamiati migeni katika maisha yao.
Lakini miongoni mwao kuna wachache wazuri na wenye wema. Kwatampola analinda utu wake licha ya majaribu mengi anayopitia kila siku. Kutokana na wema na utu wake, Kabaila Bumaali anamtunuku Kwatampola zawadi kubwa iliyokuwa ndoto yake kila siku! Kwatampola anasifiwa kwa utu wake na kufahamika kwa makabaila wengine sana. Ni kweli kwamba Chema Chajiuza!
Kinyume na Kwatampola, Injinia Bakehena anauza utu wake. Anapunja pesa za mwajiri wake. Yeye ni fisadi kamili wa nafsi na wa mali. Je, Injirfia Bakehena atafikwa na kitu gani mwishowe? Ataadhibiwa ama atanusurika adhabu za waajiri wake? Je, ni
kweli kwamba ???malipo ni duniani ahera yaenda hesabu?
Reviews
There are no reviews yet.