Description
Kwa utajiri walionao, akina Bamkuu na Bimkuu wanadhani dunia yote ni yao, kumbe kesho itawafudikiza! Mbali na utajiri wao wana maji safi na matamu. Maji nayo yanazidi kuwa utajiri kuliko utajiri, maana maji safi yanapanda bei kushinda dhahabu, kwani sasa ni adimu kupatikana. Tamaa kubwa ya pesa inayageuza maji bidhaa huku umma wa nchi hii ukikauka roho na nafsi zao kutapatapa. Watu wachache to ndio wanaozima kiu zao kwa maji safi. Sauti za umma zinaanza kubwata na kulalama. Kwanza mwendawazimu mwenye busara. Yeye anawakumbusha watu uzuri wa jadi na ubaya wa usasa. Kuna wanaomshuku na wanaomwona mwenye busara, Kisha kuna Kristy, kibinti kidogo cha Bamkuu na Bimkuu. Sauti yake ya ugonjwa ni hafifu !akin! imara na sisitizi. Kila dakika anadai dawa ya kutibu maradhi yake: map ya utakatifu wa kiwiliwili na akili, ya chemchemi ya msitu huru wa wananchi, map ambayo hayapanikani tena. Busara, binti mkubwa wa Bamkuu na Bimkuu ni msomi anayeukaripia uhifadhina na kuzikaribisha mbegu za haki za wananchi wote, hasa za wanyonge.
Reviews
There are no reviews yet.