Description
Hatua za Kiswahili Rasmi, Kitabu cha mwanafunzi ni mfululizo wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa ufundi kwa kufuata mtalaa mpya unaosisitiza umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunz: kukuza weledi wake katika stadi za kusikiliza na kuzungumza, sarufi na matumizi ya lughakusoma na kuandika. Vitabu hivi vina sifa zifuatazo:
Â
– Mada kuu zilizopangwa kwa kuzingatia ruwaza ya mtalaa ya Kiswahili Gredi ya 3 ili kurahisisha utumiaji.
– Vipindi vilivyopangwa kushughulikia mada ndogo mbalimbali kulingana na ruwaza ya mtalaa.
– Picha na michoro iliyochorwa kwa rangi za kupendeza ili kuvutia usomaji na ujifunzaji.
-Â Maswali dodoso yanayochochea uwezo wa mwanafunzi kufikiria na kudadisi masuala mbalimbali.
– Kazi za ziada na majaribio yanayomhusisha mwanafunzi binafsi, wanafunzi wawiliwawili na wanafunzi kwenye makundi katika shughuli ainaaina.
-Â Mradi wa nyumbani unaowahusisha wazazi na walezi katika ujifunzaji wa Kiswahili na pia kukuza uwajibikaji.
-Â Hadithina utajiri wa shughuli nyingine zinazokuza umilisi wa kimsingi wa lugha ya Kiswahili na zilizooanishwa na masuala mtambuko, maadili chanya miongoni mwa masuala mengine.
– Matumizi ya teknolojia kwa mfano kusikiliza sauti redioni na unasaji sauti kwa kutumia simu na vifaa vingine vya kiteknolojia.
Reviews
There are no reviews yet.