Description
Mwanazuoni anayetaka kuzama, kuchimba na kuchambua masuala muhimu yanayohusu Riwaya ya Kiswahili atakuwa amezima kiu yake baada ya kuchota kutoka kisima hiki chenye maji mengi, matamu na yaliyo salama. Ama kwa kubuni na kuandika kitabu hiki, Profesa Joshua Madumulla wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Tanzania amevinjari uwanja mzima wa Riwaya ya Kiswahili na
kutoa ufafanuzi ulio murua ikiwa ni pamoja na maana yake, historia yake, aina zake mbalimbali na misingi ya uchambuzi wake. Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake kinachokidhi haja iliryokuwepo ya ufafanuzi wa Riwaya ya Kiswahili ikiwalenga wanazuoni wa elimu ya juu hususani wale walio katika vyuo vikuu.
Reviews
There are no reviews yet.