Description
Sarufi ndio uti wa mgongo wa lugha. Kufahamu lugha ni kufahamu sarufi yake. Sarufi Fafanuzi ya Kiswahili kinafuatilia silabasi ya lugha ya Kiswahili kwa shule za sekondari na kushughulikia matawi muhimu ya sarufi kwa mapana na marefu. Haya ni kama vile aina za maneno, ngeli za nomino, vitenzi n.k. Ufafanuzi na matumizi mwafaka yamefanya yaliyomo kueleweka kwa urahisi. Vile vile mambo muhimu yanayozingatiwa katika vyuo vya walimu na vyuo vikuu yameshughulikiwa kwa kirefu. Bila shaka wale watakaokitumia kitabu hiki watanufaika vilivyo.
Baada ya kufuzu katika Chuo…Kikuu cha Nairobi, Gichohi Waihiga alifunza katika shule na vyuo kadhaa nchini Kenya kama vile Shule ya Upili ya Aga Khan (Nairobi), Chuo cha Walimu cha Kagumo na Chuo cha Walimu cha Kisii. Kwa sasa yeye ni mtayarishi wa vipindi vya kielimu kwa njia ya redio na televisheni katika Idara ya Huduma za Elimu kupitia Vyombo vya Habari (EMS), katika Taasisi ya Elimu ya Kenya. (ME).
Reviews
There are no reviews yet.